AGU CLASSIC   Blog

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

AGU CLASSIC BLOG

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

Follow Us On Instagram

28 Mar 2014

MICHEZO SMMMCo - MASOKA- KIVIMBI CHA MASHINDANO YA INTERCLASSES CHATIMKA LEO

Ligi ya mpira wa miguu  maarufu kama soka inayopigwa katika chuo kikuu cha Tumaini - SMMUCo- katika kampasi ya  Masoka imeendelea jioni ya leo tarehe 28 March 2014 katika kiwanja kikubwa cha Kirima maeneneo ya Kibosho katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo katika mchezo wa leo ulizozikutanisha timu ya Mwaka wa 3 ambao walikuwa nyumbani dhidi ya timu Mwaka wa kwanza ambao wameonekana kuwa tishio kubwa katika mashindano hayo.

Mchezo ulianza kwa kasi na vizuri kwa mwaka wa kwanza katika kipindi cha kwanza kwani waliweza kucheza vizuri na kumiliki mpira vizuri kwa safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na vijana wadogo kama Walter,Agrey ,Doa na Joe  na kuweza kupata goli lililofungwa kwa shuti kali lililopigwa na Joe na kumshinda mlinda mlango Isa Mkandarasi wenyewe hupenda kumuita ISA MIUJIZA goli hilo lilidumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanzaa,,Hali ilibadilika kipindi cha pili ambapo wakongwe wa soka chuoni hapo mwaka wa 3 kufanya mabadiliko ambayo yalibadilisha hali 
ya mchezo na kufanikiwa kulishambulia lango la timu pinzani kama nyuki.

Ghafla .... uwanja wa mpira wa miguu uligeuka kuwa uwanja wa mabishano, makubaliano,makonde na ubabe baada ya kuzuka tafrani kutokana na kutoelewana kwa waamuzi wa mchezo huo baada ya mchezaji wa mwaka wa kwanza kunawa mpira katika eneo la hatari na mwamuzi wa pembeni kuamuru kuwa ni penalti jambo lililokataliwa vibaya mno na vijana wa mwaka wa kwanza na kupelekea kususia mchezo huo hali iliyomfanya mwamuzi kumaliza mchezo na kuwapa ushindi laini (wa mezani) timu ya mwaka wa tatu kwa kupata pointi tatu muhimu zilizowafanya waongoze ligi hiyo kwa kuwa na pointi 9 na kuwa mabingwa wa ligi hiyo.

Kilichofatia uwanjani hapo ni shangwe kubwa la mwaka wa tatu walozunguka maeneo kibao ya chuo na yaliyojirani na chuo huku wakiimba , kucheza na kuruka ruka huku na kule hadi mida ya usiku .

Hebu fanya kushuhudia angalau picha ya washabiki hao wakiwa katika buuuuuuuuuuuruuuuuuuuuudaaaaaaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..................................





                                          Hicho kimbembe kiliendelea hadi usiku bila kuchoka


              Baadhi ya wadau wa soka wa mwaka wa 3 wakiwa katika pozi zenye nyuso za furaha

No comments:

Post a Comment