Timu ya mpira wa miguu (soka ) ya Mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Tumaini Makumira (SMMUCo) imefufua matumaini makubwa ya kusonga mbele katika ligi inayoendelea chuoni hapo baada ya kuibuka na ushindi MKUBWA wa magoli manne (4) kwa bila dhidi ya mwaka wa pili, Timu hiyo ambayo ilpoteza mchezo wake wa kwanza ugenini dhidi ya Mwaka wa kwanza sasa inaongoza msimamo wa ligi ikiwa ina pointi 3 na magoli 5 ikifatiwa na mwaka wa kwanza nao pia wakiwa na point 3 na magoli mawili.
Kapu la magoli lilianza mapema kabisa kipindi cha kwanza kwa magoli ya Joseph Mgaya , Masangula na Herny Mtewere maarufu kama HAKUNAGA , na kipindi cha pili mchezaji Joshua Simon( HOME BOY) alishindilia goli la 4 kwa shuti kaliiiii, ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumatatu na kuzikutanisha timu za Mwaka wa pili na Mwaka wa kwanza.
Pia katika mchezo wa Volleyball kesho kutakuwa na mchezo kati ya Mwaka wa tatu dhidi ya Mwaka wa pili huku Mwaka wa tatu wakiwa wanaongoza pia baada ya jana kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya mwaka wa kwanza
Cheki picha mbalimbali jinsi ilivyokuwa kwenye uwanja wa Kirima Sec
Ukitaka ma photo nini tuonane au sio
safi sana agu aka mafuvu
ReplyDeletepamoja xana axeeeeee
Delete