Ni siku ya Jumapili tarehe 10 / 8 / 2014 wanajeshi wa DAKAWA maarufu kama MABAIBO UNIT toka pande za Ipuli pembezoni mwa barabara iendayo magereza watafanya BONGE ya Show , Bonge ya Party katika kusheherekea miaka 8 tangu kuanzishwa kwa CREW hiyo.
Mpango mzima wa sherehe utaanza mishale ya saa 9:00 Alasiri hadi choka mwenyewe yanii Kokorikoooooo BUREEEEEEE katika viwanja vyao ( barabara ya magereza ) huku kukiwa na burudani za kutosha kutoka kwa wasanii mbalimbali wa mkoa wa Tabora na nje ya mkoa ambao
watawasha MOTO NA KUAMSHA POPO kwenye JUKWAA hilo bila kusahau wale wazee wa kuvunjaaa viungo vya mwili yaaani Mashakers - Madancer kibao toka mkoani Tabora nao pia watakuwepo kwenye show ili kutoa BURUDANI kwa MASHABIKI watakaohudhuria SHOW hiyo.
Hii sio ya kukosaa wala kuadisiwa na si tu kwa BURUDANI kwa raia watakaohudhuria bali kupitia burudani hizo watu WATAELIMIKA kuhusu baadhi ya mambo na kupata elimu bora kuhusu MAISHA KWA UJUMLA
MABAIBO UNIT INAWAKARIBISHA MASHABIKI WAKE WOOOTE NA WATU WOOTE WANAOPENDA BURUDANI MKOANI TABORA KUFIKA BILA KUKOSA SIKU HIYO
_________________________________________________
Ahsante kwa kutembelea blog yetu kuwa mwanafamilia kwa kutu follow
Facebook - like page yetu @ Agu Classic
Twitter - @ AugustinoDamson
Facebook - @ Augustino Kaulule Agu classic
Instagram - @ aguclassic
Whatsup - 0753825788
No comments:
Post a Comment