Baada ya kupotea kwa mashindano ya pamoja ya vituo vya Klasta ya Nzega tangu mwezi June 2021, Idara ya Michezo ikiongozwa na ndugu Alfred Masele (Mratibu wa FPCT Tazengwa) na Augustino Kaulule (Mratibu wa Moravian Ushirika) ilikaa chini na kubuni njia rafiki itakayosaidia kurudisha Upendo, Umoja na Amani baina ya watoto, watendakazi na jamii nzima inayozunguka vituo hivyo vitano kwa Kuanzisha MICHEZO YA KIRAFIKI UPANDE WA FOOTBALL, NETBALL NA RIADHA ITAKAYOFANYIKA KILA JUMAMOSI, KUANZIA MWEZI WA PILI NA KUENDELEA.
Mchungaji Peter S. Mhekela akizindua michezo ya kirafiki kwa kuzungumza na wachezaji na viongozi wa Vituo vya Moravian Ushirika - TZ0564 na TAG Itobo
Kwa mujibu wa ratiba, Michezo hiyo ilipangwa kuanza tarehe 12/02/2022, Lakini kutokana na hali mbaya ya hewa Michezo ya kwanza kati ya Moravian Ushirika dhidi ya TAG Itobo haikufanyika. Hivyo basi michezo ilisogezwa Jumamosi ya tarehe 19/02/2022 kwa kuzinduliwa rasmi na MCHUNGAJI MWENYEJI WA KANISA LA MORAVIAN USHIRIKA , MCHUNGAJI: PETER SAMSON MHEKELA.
Na katika michezo hiyo ya awali kituo cha Moravian Ushirika kiliibuka na ushindi kwa michezo yote yaani Mpira wa Miguu 6-1 na Mpira wa Pete 42-5
Mchezo wa Netball ukiendelea |
Mchezo kati ya Ushirika na Itobo ukiendelea (Football) |
Lengo la michezo hii ni kukuza upendo, umoja na amani, hii ni picha ya pamoja iliyojumuisha wachezaji na viongozi wa Ushirika na Itobo |
Hali kadhalika michezo hii itaendelea Jumamosi hii ya tarehe 26/02/2022 kwa mchezo mmoja ambapo TAG Itobo watakuwa mwenyeji dhidi ya TAG Ipilili
whatsaap - 0753825788
Instagram: moravian_ushirika_academy
Facebook: Moravian Ushirika Academy
No comments:
Post a Comment