AGU CLASSIC   Blog

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

AGU CLASSIC BLOG

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

Follow Us On Instagram

6 Aug 2021

ASKOFU EZEKIEL YONA WA 'KMTM' AZINDUA OFISI YA WATENDAKAZI WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANA MORAVIAN USHIRIKA - NZEGA

 


Jumapili ya tarehe 01/08/2021ilikuwa ni Jumapili ya kipekee na yenye furaha kwa waumini wa kanisa la Moravian Ushirika Nzega. Baada ya kutembelewa na ugeni mkubwa wa vongozi wa juu wa jimbo la Kanisa la Moravian Tanzania Magharibi (KMTM) wakiongozwa na Baba Askofu Ezekiel Yona.

Pamoja na kuongoza ibada ya Jumapili hiyo, Baba Askofu Ezekiel Yona alizindua Ofisi ya watendakazi wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana Moravian Ushirika chenye

namba za Usajili TZ0564, Ofisi hiyo yenye vyumba Vitano, ambayo imegharimu zaidi ya Tsh 22,000,000 ilianza kujengwa tarehe 01/09/2019 na Kanisa hilo mara tu baada ya kupokea Huduma ya Mtoto na Kijana.

Baba Askofu, kwa pekee aliwapongeza viongozi wa Kanisa chini ya Mchungaji Kiongozi Peter Samson Mhekela kwa ujenzi wa ofisi nzuri na ya kisasa ya Watendakazi, huku akitoa wito kwa viongozi wa kanisa na Mratibu wa Kituo hicho kuzidi kufanya Maendeleo ya miundombinu ya kanisa na kituo kwa ujumla.

Ofisi ya Watendakazi wa kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana Moravian Ushirika - TZ0564

Pamoja na hayo Baba Askofu anaamini kuwa kuwepo kwa Ofisi nzuri na ya kisasa kwa Watendakazi wa Kituo hicho kutapelekea kupatikana kwa Mawazo na Mipango mizuri ya kimaendeleo hasa katika kuwakomboa watoto na vijana katika Umaskini kwa Jina la Yesu. Hivyo aliwataka watendakazi hao Augustino Kaulule (Mratibu), Sarah Luhamba (Mhasibu) na Jenipher J. Aroko (Mwanajamii) kutumia fursa hiyo ya kuwa na Ofisi nzuri kuhakikisha wanawakomboa watoto na vijana katika umaskini na kuleta maendeleo ya Kituo na Kanisa kupitia mawazo na mipango mizuri itakayobuniwa ofisini humo na kutekelezwa ipasavyo.


VIDEO| Zoezi zima la uzinduzi wa Ofisi ya Watendakazi Moravian Ushirika

Ukiachana na uzinduzi wa Ofisi ya watendakazi, Pia baba askofu alifanya uzinduzi wa Gari mpya ya kanisa aina ya KLUGEL “L” Rangi nyeusi yenye namba za usajili T 368 DVT ambayo imegharimu kiasi cha zaidi ya Tsh 23,500,000 ambayo itatumika na kanisa katika kulitangaza na kulieneza neno la Mungu sehemu mbalimbali ili kuhakikisha watu wanalipokea na kumpokea Yesu Kristo katika Maisha yao.

Baba Askofu Ezekiel Yona akizindua gari jipya la Kanisa 



TANGAZA NASI


No comments:

Post a Comment