AGU CLASSIC   Blog

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

AGU CLASSIC BLOG

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

Follow Us On Instagram

6 Aug 2021

TIMU YA MORAVIAN USHIRIKA ACADEMY KUINGIA KAMBINI RASMI KUJINOA NA MCHEZO WA KIRAFIKI DHIDI YA MORAVIAN USOKE YA URAMBO

 


Timu ya mpira wa Miguu kutoka kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana cha Moravian Ushirika Nzega – TZ0564 Moravian Ushirika Academy, inajiandaa kuingia kambini rasmi kwa ajili ya Mchezo wa Kirafiki dhidi ya timu ya Mpira wa Miguu kutoka kituo cha Moravian Usoke kilichopo wilayani Urambo Mkoani Tabora.

Akizungumza moja kwa moja na Mwandishi wetu, Kocha Mkuu wa timu ya Moravian Ushirika Christopher Kaombwe maarufu kama Chris Gomez Mpili,

Aliushukuru uongozi wa kituo cha Moravian Usoke kwa kuona umuhimu wa Michezo kwa watoto hadi kupelekea kuomba mechi ya kirafiki, kwani kupitia michezo watoto huimarika  Afya zao, hufahamiana, kukuza kipaji cha mpira wa Miguu kwa watoto na Vijana na mwisho itatoa fursa kwa viongozi wa pande zote mbili kujifunza namna bora ya kuwalea watoto na kuwakomboa kutoka kwenye Umasikini kupitia michezo na njia nyinginezo ambazo zinatumika vituoni. Pamoja na hayo Kocha Mkuu alimwambia mwandishi wetu kuwa Kikosi chake kitaingia kambini rasmi wiki ijayo kwa ajili ya mazoezi ya kujiwinda na mchezo huo ambao utapigwa mapema Mwezi wa Tisa katika kiwanja cha Moravian Ushirika alimaarufu ‘’ Kwa Mhekela’’.


Upande mwingine Nahodha Mkuu, Samson Emanuel na Kipa, Julias Emanuel wa Moravian Ushirika Academy, kwa pamoja wameonesha furaha yao kufuatia taarifa hiyo ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Moravian Usoke iliyowasilishwa rasmi kituoni na Mratibu wa Kituo cha Usoke Ndugu Elikana William. Pia nahodha wa timu alisema wapo tayari na mchezo huo wa kirafiki kwa kuingia kambini na kujinoa lakini pia kwa kuwaombea watoto/vijana wenzao wa Usoke Afya njema, Mipango mizuri na safari njema kwa ajili ya kufanikisha yote.

Samson Emmanuel (Nahodha wa Moravian Ushirika Academy)

Julius Emmanuel - Goli kipa wa Moravian Ushirika Academy


TANGAZA NASI.....

No comments:

Post a Comment