Rais Obama ameelezea furaha yake ya
kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na kutenda kulingana
na injili anayoihubiri.
Maswala mbali mbali yenye umuhimu wa kimataifa pamoja na kidini huenda yakajadiliwa katika mkutano huo.
Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya
kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na
kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani.
Papa Francis amekuwa mstari wa mbele akipigania
kubadili sera na mtazamo wa Kanisa na viongozi duniani kuhusiana na
mikakati ya kupunguza tofauti kubwa baina ya maskini na matajiri duniani
.
Aidha viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo Nchini Ukraine, na swala la upatikanaji wa amani mashariki ya kati.
Mwafaka baina ya mitazamo tata ya wawili hao
kuhusiana na maswala ya uavyaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi
na ndoa ya jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada
itakayojadiliwa .
Baada ya kukutana na papa rais Obama ameratibiwa
kukutana na rais wa Italia Giorgio Napolitano mbali na waziri wake mkuu
Matteo Renzi.
Obama amezuru Roma baada ya siku tatu ya
mazungumzo na viongozi wa Uholanzi na Umoja wa ulaya huko Brussels
ambapo mada kuu ilikuwa ni taharuki inayokumba eneo zima la Crimea na
Ukraine
baada ya Urusi kutuma vikosi vya jeshi lake katika jimbo hilo .
Obama tayari ameanza kuandaa mikakati na vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kwa kuingia Ukraine.
Obama ameambatana na waziri wake wa maswala ya kigeni John Kerry.
SOURCE YA HABARI HII NI KUTOKA BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment