Maafisa wa utawala katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya
Congo wametangaza siku tatu kuomboleza wakimbizi waliofariki katika
ajali ya boti katika ziwa Albert siku ya Jumamosi.
Boti hiyo, ilikuwa inawasafirisha wakimbizi wa DRC kutoka nchini Uganda wakirejea nchini mwao.
Inaarifiwa boti hiyo ilikuwa imebeba abiria
zaidi ya inavyoweza kumudu na maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu
miambili hamsini waliOkuwa wameabiri boti hiyo walizama.
Serikali ya Uganda ilisema kuwa iliweza kupata
maiti 107 ikiwemo watoto 57 baada ya bnoti hiyo kuzama. Wote walikuwa
wanatarajiwa kufika salama nyumbani DRC.
Walikuwa wanaishi katika kambi za wakimbizi nchini Uganda na inaarifiwa watu 300 walikuwa wameabiri boti hiyo illipozama.
No comments:
Post a Comment