AGU CLASSIC   Blog

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

AGU CLASSIC BLOG

BLOG PENDWA YA MUZIKI, HABARI, MICHEZO & BURUDANI, WATOTO NA VIJANA. Instagram| AguClassic, WhatsUp| +255753825788, YouTube| Agu Classic TV, Email| damsonaugustino@gmail.com

Follow Us On Instagram

6 Sept 2014

SOKA - MZUNGUKO WA PILI LIGI DARAJA LA 4 MKOANI TABORA UNAANZA LEO, MWENGE FC NA STAND FC DIMBANI

Baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi daraja la nne (4) mkoani Tabora kumalizika wiki kadhaa zilizopita ligi hiyo inaendelea leo tarehe 6/9/2014  kwa mzunguko wa pili kwa kuzikutanisha timu za Mwenge FC na Stand FC katika uwanja wa VITA mkoani Tabora mishale ya saa Kumi na nusu 10:30 Jioni . Mechi inatabiliwa na wapenzi wengi wa soka mkoani hata baadhi ya wachezaji kuwa ni mechi ngumu kwa pande zote mbili kutokana na
uimara wa timu zote mbili ambapo katika mchezo wa kwanza timu ya Stand ilipoteza mchezo wake kwa magoli 4-3 hivyo leo watahitaji kupambana kwa nguvu zote ili kuweza kulipiza kisasi na kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo nao Mwenge FC ambao walioibuka washindi katika mchezo wa awali  nao wanahitaji ushindi ili kuendelea kujikita kileleni katika kundi lao,
Mlinzi (beki) wa timu ya Mwenge Karim Pazz alisema" wamejiandaa vizuri na mchezo wa leo kwani wanaitambua vizuri timu ya Stand kuwa ni moja ya timu nzuri mkoan Tabora pia alisisitiza kujitokeza kwa mashabiki wengi wa timu yao kwenda kushabikia mchezo huo kwani itaongeza hamasa  ya mchezo kwa wachezaji"

Kwa hiyo wapenzi wa soka mkoani Tabora msikose mchezo huo wa kusisimua utakaopigwa leo tarehe 6/9/2014 saa 10:30 ndani ya uwanja wa Vita 

_________________________________________________________________

Ahsante kwa kutembelea blog yetu kuwa mwanafamilia kwa kutu follow
Facebook - like page yetu  @ Agu Classic
Twitter   - @ AugustinoDamson
Facebook  - @ Augustino Kaulule Agu classic
Instagram - @ aguclassic

Whatsup   - 0753825788

No comments:

Post a Comment