MKOPO WA ELIMU
Kwa kutambua umuhimu wa elimu katika jamii ya sasa , Mfuko wa PSPF umebuni huduma huduma ya mkopo wa elimu kwa ajili ya wanachama wake kujiendeleza kielimu, Mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote ile ya elimu mfano stashahada , shahada, shahada ya uzamili au hata mafunzo ya ufundi. Mfuko utagharamia ada kwa kipindi chote cha masomo ya mwanachama.
VIGEZO VINAVYOZINGATIWA
- Mwanachama kuwa amethibitishwa na mwajiri
- Mwanachama awe amekubaliwa kujiunga na chuo cha ndani au nje ya nchi
- Mwanachama awe na kibali cha mwajiri
- Mwanachama awe amechangia angalau miezi 24
FANYA MAAMUZI SAHIHI, JIUNGE NA PSPF KWA TULIZO LA MAISHA YAKO.
No comments:
Post a Comment