Jumapili
ya tarehe 01/08/2021ilikuwa ni Jumapili ya kipekee na yenye furaha kwa waumini
wa kanisa la Moravian Ushirika Nzega. Baada ya kutembelewa na ugeni mkubwa wa vongozi
wa juu wa jimbo la Kanisa la Moravian Tanzania Magharibi (KMTM) wakiongozwa na
Baba Askofu Ezekiel Yona.
Pamoja na kuongoza ibada ya Jumapili hiyo, Baba Askofu Ezekiel Yona alizindua Ofisi ya watendakazi wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana Moravian Ushirika chenye
namba za Usajili TZ0564, Ofisi hiyo yenye vyumba Vitano, ambayo imegharimu zaidi ya Tsh 22,000,000 ilianza kujengwa tarehe 01/09/2019 na Kanisa hilo mara tu baada ya kupokea Huduma ya Mtoto na Kijana.Baba
Askofu, kwa pekee aliwapongeza viongozi wa Kanisa chini ya Mchungaji Kiongozi
Peter Samson Mhekela kwa ujenzi wa ofisi nzuri na ya kisasa ya Watendakazi,
huku akitoa wito kwa viongozi wa kanisa na Mratibu wa Kituo hicho kuzidi
kufanya Maendeleo ya miundombinu ya kanisa na kituo kwa ujumla.
Ofisi ya Watendakazi wa kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana Moravian Ushirika - TZ0564 |
Pamoja
na hayo Baba Askofu anaamini kuwa kuwepo kwa Ofisi nzuri na ya kisasa kwa
Watendakazi wa Kituo hicho kutapelekea kupatikana kwa Mawazo na Mipango mizuri
ya kimaendeleo hasa katika kuwakomboa watoto na vijana katika Umaskini kwa Jina
la Yesu. Hivyo aliwataka watendakazi hao Augustino Kaulule (Mratibu), Sarah Luhamba
(Mhasibu) na Jenipher J. Aroko (Mwanajamii) kutumia fursa hiyo ya kuwa na Ofisi
nzuri kuhakikisha wanawakomboa watoto na vijana katika umaskini na kuleta
maendeleo ya Kituo na Kanisa kupitia mawazo na mipango mizuri itakayobuniwa
ofisini humo na kutekelezwa ipasavyo.
VIDEO| Zoezi zima la uzinduzi wa Ofisi ya Watendakazi Moravian Ushirika
Ukiachana
na uzinduzi wa Ofisi ya watendakazi, Pia baba askofu alifanya uzinduzi wa Gari
mpya ya kanisa aina ya KLUGEL “L” Rangi nyeusi yenye namba za usajili T 368 DVT ambayo
imegharimu kiasi cha zaidi ya Tsh 23,500,000 ambayo itatumika na kanisa katika
kulitangaza na kulieneza neno la Mungu sehemu mbalimbali ili kuhakikisha watu
wanalipokea na kumpokea Yesu Kristo katika Maisha yao.
Baba Askofu Ezekiel Yona akizindua gari jipya la Kanisa |
No comments:
Post a Comment