Timu
ya mpira wa Miguu kutoka kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana cha Moravian
Ushirika Nzega – TZ0564 Moravian
Ushirika Academy, inajiandaa kuingia kambini rasmi kwa ajili ya Mchezo wa
Kirafiki dhidi ya timu ya Mpira wa Miguu kutoka kituo cha Moravian Usoke
kilichopo wilayani Urambo Mkoani Tabora.
Akizungumza moja kwa moja na Mwandishi wetu, Kocha Mkuu wa timu ya Moravian Ushirika Christopher Kaombwe maarufu kama Chris Gomez Mpili,
Aliushukuru
uongozi wa kituo cha Moravian Usoke kwa kuona umuhimu wa Michezo kwa watoto hadi
kupelekea kuomba mechi ya kirafiki, kwani kupitia michezo watoto huimarika Afya zao, hufahamiana, kukuza kipaji cha mpira
wa Miguu kwa watoto na Vijana na mwisho itatoa fursa kwa viongozi wa pande zote
mbili kujifunza namna bora ya kuwalea watoto na kuwakomboa kutoka kwenye
Umasikini kupitia michezo na njia nyinginezo ambazo zinatumika vituoni. Pamoja
na hayo Kocha Mkuu alimwambia mwandishi wetu kuwa Kikosi chake kitaingia
kambini rasmi wiki ijayo kwa ajili ya mazoezi ya kujiwinda na mchezo huo ambao
utapigwa mapema Mwezi wa Tisa katika kiwanja cha Moravian Ushirika alimaarufu
‘’ Kwa Mhekela’’.
Upande
mwingine Nahodha Mkuu, Samson Emanuel
na Kipa, Julias Emanuel wa Moravian
Ushirika Academy, kwa pamoja wameonesha furaha yao kufuatia taarifa hiyo ya
mchezo wa kirafiki dhidi ya Moravian Usoke iliyowasilishwa rasmi kituoni na Mratibu wa Kituo cha Usoke Ndugu Elikana
William. Pia nahodha wa timu alisema wapo tayari na mchezo huo wa kirafiki
kwa kuingia kambini na kujinoa lakini pia kwa kuwaombea watoto/vijana wenzao wa
Usoke Afya njema, Mipango mizuri na safari njema kwa ajili ya kufanikisha yote.
Samson Emmanuel (Nahodha wa Moravian Ushirika Academy) |
Julius Emmanuel - Goli kipa wa Moravian Ushirika Academy |
TANGAZA NASI..... |
No comments:
Post a Comment