Vijana kutoka kanisa la Moravian Ushirika linalopatikana wilaya ya Nzega - Tabora, wameanza rasmi mazoezi ya nguvu kujiwinda na mashindano ya CCT CUP ambayo
yanajumuisha makanisa yote ya CCT Nzega Mjini yatakayoanza tarehe 17/01/ 2019.
Vijana hao kutoka kanisa la Moravian Ushirika watashiriki kwenye michezo miwili yaani Mpira wa Miguu (Football) na Mpira wa Pete (Netball). Kwa upande wao wachezaji wa Mpira wa miguu wameridhishwa na mazoezi ambayo yanaendelea kila siku kambini, huku Captain wa timu hiyo Eliud na Captain Msaidizi Toddy wamewaomba vijana kuzidi kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kupata wachezaji wengi zaidi lakini pia kusapoti wachezaji wakati wa mazoezi na kujenga ushirikiano zaidi baina yao.
Kamati ya ufundi ikiongozwa na mtaalamu Lukas imejinadi pia kuwa ipo vizuri kabisa kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoanza Jan 17 na kuthibitisha kuwa Timu zao zitatoa kichapo kwa kila timu pinzani itakayo katiza mbele ya macho yao.
Upande wa wadada (Netball) Nao pia wametoa shukran zao za dhati kwa wachezaji wanaondelea kuripoti kambini kwa ajili ya mazoezi na kwa mashabiki na wadau mbalimbali wanaojitokeza kusapoti kushauri n.k . Lakini pia wanazidi kuwaomba Wadau na vijana zaid kuzid kujitokeza kambini ili kuwa pamoja na kusapoti timu hizo.
No comments:
Post a Comment